December 12, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Samia afanya tena mabadiliko ya baraza la mawaziri

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri pamoja na kubadilisha muundo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo Sekta ya Habari ameirejesha kwenye Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mabadiliko hayo yamefanyika leo tarehe 8 Disemba 2024 na Mawaziri hao wataapishwa tarehe 10 Disemba, 2024, kwenye Ikulu Ndogo ya Tunguu Zanzibar.

Rais Samia kupitia taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu amemteu Jerry Silaa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo awali alikuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Pia amemteua Profesa Palamaganda Kabudi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais Samia amemteua Abdallah Ulega kuwa Waziri wa Ujenzi akichukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hapo awali Ulega alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambapo nafasi hiyo imechukuliwa na Dk. Ashatu Kijaji.

Taarifa hiyo inasema kuwa Rais Samia amemhamisha Wizara Dk. Damas Ndumbaro kwenda kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, wakati hapo Awali Dk. Ndumbaro alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais amemteuwa Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukua nafasi ya Hamadi Masauni, awali Bashungwa alikuwa akihudumu kama Waziri wa Ujenzi.

Rais Samia amefanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri na viongozi mbalimbali ambapo amemtua Mhandisi Hamad Masauni kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hapo awali Masauni alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani, nafasi ambayo imechukuliwa na Innocent Bashungwa akitokea Wizara ya Ujenzi.

Rais Samia, amemteua Dk. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi akichukua nafasi ya Abdallah Ulega ambaye emeteuliwa kuwa Waziri kwenye Wizara ya Ujenzi.

Rais Samia amefanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali, ambapo amemteuwa tena Gerson Msigwa kuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, akichukua nafasi ya Thobias Makoba ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Wakati huo huo Rais Samia amefanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali ambapo amewateuwa Mobhare Matinyi na Thobias Makoba kuwa mabalozi, ambao kwa taarifa iliyotolewa na Ikulu watapangiwa vituo vya kazi hapo baadae.

Wawili hao kwa Nyakati tofauti walihudumu kwenye nafasi ya Msemaji wa Serikali na Mkuu wa Idara ya Habari na Maelezo.

Pia Rais amemteua Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohammed Janabi kuwa mshauri Rais wa Masuala ya Afya na Tiba huku akiendelea na majukumu yake kama mkurugenzi wa Hospital ya Muhimbili.

About The Author

error: Content is protected !!