December 22, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Waliotaka kumteka Tarimo waburuzwa kortini

 

WATUHUMIWA sita wamefikishwa katika Mahakama Hakimu Mkazi Kivukoni iliyopo Kinondoni kwa kosa la kutaka kumteka mfanyabiashara Deogratius Tarimo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Watuhumiwa ni pamoja na:- Bato Bahati Tweve, Nelson Elmusa, Anitha Alfred Temba, Isaack Mwaifuani, Fredrick Juma Msatu na Benki Daniel Mwakalebela.

Akiwasomea shtaka moja kwa watuhimiwa hao wakili wa Serikali John Mwakifuna mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Ramadhani Rugemalila , amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la utekaji .

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Kiluvya, jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba 2024. Wanadaiwa kutendo kosa hilo la kutaka kumteka na kumweka kizuizini kinyume na utararibu.

Mwakifuna alidai kitendo ni kinyume cha sheria fungu namba 381 (1) cha kanuni kanuni ya adhabu.

Mahakama hiyo imeweka wazi dhamana hao wakitakiwa wawe na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya shilingi 10 Milioni . Watuhumiwa hao kwa pamoja wamekana shtaka hilo. Shauri litatajwa tena tarehe 19 Desemba 2024.

About The Author

error: Content is protected !!