MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo, amepatikana usiku huu baada ya kutupwa karibu na makao makuu ya chama hicho, Magomeni, Dar es salaam, akiwa na majeraha na mahututi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Ado Shaibu, katibu mkuu wa chama hicho, amethibitisha kupatikana kwa kiongozi huyo na kuongeza, “hali ya kiafya ya Nondo ni mbaya.”
Mwanaisasa huyo kijana alitekwa majira ya asubuhi ya leo Jumapili, tarehe 1 Desema 2024 na wanaoitwa na serikali, “watu wasiofahamika.”
Tukio hilo lilitokea katika stendi ya Magufuli Mbezi Luis, wakati Nondo akitokea mkoani Kigoma kwa basi alikokuwa akishiriki shughuli za uchaguzi.
“Nondo amepatikana akiwa na majeraha ambayo yametokana na vipigo na sasa anapelekwa Hospitali akiwa mahututi,” ameeleza Ado katika mahojiano yake na MwanaHALISI Online.
ZINAZOFANANA
Wamilikiwa Jengo la Kariakoo wapandishwa kizimbani kwa mauaji bila kukusudia
Mahakama yamuachia huru aliyekuwa RC Simiyu
Chadema yaita Kamati Kuu ya dharura kujadili uchaguzi