JOPO la Mawakili linalomtetea Boniface Jacob ‘Boni yai’ aliyekuwa Meya wa Manspaa ya Ubungo linaloongozwa na wakili Peter Kibatala umeitaka upande wa Jamhuri kukamilisha upelelezi wa kesi ya kuchapisha taarifa za uongo inayomkabili ‘Boni yai’. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yamejiri leo tarehe 21 Novemba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Franco Kiswaga baada ya Wakili wa Serikali Judith Kyamba kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.
Kibatala amedai mahakamani hapo kwa kuwa Jamhuri imemkamata na kumfikisha mahakama walipaswa kukamilisha upelelezi kama ambavyo sheria inavyotaka.
Wakili Kyamba amedai kuwa upande huo unaendelea na uchunguzi ili kukamilisha kukamilisha kwa wakati.
Hakimu Kiswaga ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 19 Desemba 2024.
Boni yai anashitikiwa mahakamani hapo kwa hati yenye mashtaka mawili ya kuchapisha habari za uongo kupitia mtandao wa X
ZINAZOFANANA
Kulikobaki ni CCM tu, wananchi pigeni kura ya hapana
Gavu: CCM imejipanga kuwatumikia wananchi, chagueni wagombea wetu
Chadema wamesema hawana ilani – Makala