KIONGOZI wa Chama (KC) wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewaonya wagombea wa chama hicho watakaochaguliwa kuwa viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa watakaochaguliwa wasiwadhulumu wananchi kwa kudai fedha. Anaripoti Salehe Mohamed, Dar es Salaam … (endelea).
Zitto amesema chama chake hakitasita kuwafukuza viongozi watakaobainika kuwatoza fedha wananchi wanapokwenda kwenye ofisi zao kupata huduma za bure.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ilani ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27, Novemba mwaka huu.
“Tumekubaliana hakuna kutoza chochote katika ofisi za serikali ya mitaa, vijiji na vitongoji, mtu anapokwenda kupatiwa huduma, atakayekwenda kinyume, atafukuzwa pasi na huruma wala woga” amesema
“Chama chetu hakina nafasi ya watu wasio na uadilifu wenye dhamira ya kuwaumiza wananchi kwa masilahi binafsi.Tumejitofautisha na wengine” amesema
tamfukuza ili akatafute chama cha kufanya anavyotaka.
ACT-Wazalendo wamedhamiria kuonyesha mfano bora wa uongozi na jambo hilo litatimia iwapo wananchi watawachagua wagombea wao katika uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika siku chache zijazo.
“Kuna wagombea wetu kwenye maeneo machache lakini tutawaonyesha wananchi tofauti yetu na hivyo vyama vingine na hivyo ndivyo tutakavyofanya pia wakituchagua tuongoze nchi mwaka 2025” amesema.
Zitto amesema wanaouchukulia uchaguzi wa serikali za mitaa kwa namna ya kipekee ndiyo maana wamekuja na ilani yake
“Nawasihi ndugu zangu kama umeshinda kwenye mtaa, chukulia kwamba ndio rais wa ACT Wazalendo ungependa kuongoza vipi nchi, ndio uongoze mtaa kwa namna hiyo” amesema
Ameongeza kuwa ACT- Wazalendo imejiandaa na uchaguzi huo, ndio maana tangu mwaka 2022 viongozi wakuu wamekuwa wakifanya ziara maeneo ya vijiji kwa ajili ya maandalizi ya mchakato huo.
Hatukujiandaa kisiasa bali, mawazo ya kwenda kwa wananchi, ndicho tulichokifanya leo kuzindua ilani ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
ZINAZOFANANA
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema
John Tendwa afariki dunia