MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akiongea na waandishi wa habari mapema leo ametoa taarifa ya maendeleo ya uokoaji ambapo amesema toka usiku hadi asubuhi ya saa moja kamili wameokolewa watu 5, tayari wameshapekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
RC Chalamila amesema taarifa yake ya awali ya uokozi ilionyesha watu 70 walishaokolewa na taarifa ya usiku hadi asubuhi tayari wameshaokolewa 5 na kufanya jumla ya watu 75 hadi kufikia saa moja asubuhi ya leo.
Aidha RC Chalamila amewatoa hofu wanaosema zoezi la uokoaji linakwenda taratibu ambapo uokozi unafanywa kwa kutumia akili na ustadi zaidi ili kutokuleta madhara zaidi na ndio maana idadi ya wanaokolewa wakiwa hai ni kubwa zaidi kuliko waliopeza maisha.
Hivyo wananchi waendelee kuwa watulivu vifaa vyote vya uokozi vipo zoezi linaendelea kwa umakini mkubwa ili kuokoa maisha ya wapendwa wetu wafanyabiashara walioko katika jengo hilo
ZINAZOFANANA
Prof. Kitila: Lissu ameudanganya Umma, hatukupanga mapinduzi
Samia atambuliwa miongoni mwa Wanawake 100 wenye nguvu zaidi Duniani na Forbes
TMA yatoa tahadhari uwepo wa kimbunga Chido