KIONGOZI wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu amezindua Ilani ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Ilani hiyo imezinduliwa leo Novemba 17, 2024 katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni Dar es salaam. Waliohudhuria katika uzinduzi huo ni pamoja na wagombea wa walioenguliwa na waliobakishwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi na Vitongoji.
Wakati akitoa hotuba yake, Dorothy Semu amesema, “leo tunazindua ilani. Kwa hivyo ni siku ya kihistoria katika nchi yetu; siku ambayo inaweka utamaduni mpya wa kisiasa katika kuendea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Uchaguzi huu hatuendi kuukabili kwa maneno matupu.”
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji utafanyika nchini Novemba 27, 2024.
ZINAZOFANANA
Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi
Mbowe, Lissu wawagawa viongozi wa Kigoma
Rais Samia kwenda na Dk. Nchimbi 2025