SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati imeanzisha mkakati wa kitaifa unaolenga kupunguza vifo vinavyotokana na matumizi ya kuni kwa kupikia, huku ikilenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia. Mradi huu unatekelezwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), na unalenga kuboresha afya za wananchi na kulinda mazingira. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).
Matumizi ya kuni kwa kupikia yamesababisha madhara makubwa ya kiafya, na kila mwaka, takribani watu milioni 4.3 duniani wanapoteza maisha kutokana na magonjwa yanayosababishwa na moshi wa kuni, kama vile kifua kikuu, pumu, na bronchitis. Aidha, matumizi haya yanachangia uchafuzi wa hewa na uharibifu wa misitu, hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi wa Nishati Safi na Salama ya Kupikia katika Shule ya Sekondari Morogoro, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk. James Matarajio, alisisitiza kuwa mkakati huu utapunguza matumizi ya kuni, hasa kwa wanawake na watoto, na kuboresha afya zao. Mradi huu pia unalenga kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kama gesi ya kupikia, briquettes, na bio-gas, ambazo ni salama kwa afya na hazichafui mazingira.
Katika maeneo mengi ya vijijini, watu bado hutegemea kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia, jambo linaloathiri afya zao na mazingira. Kwa hivyo, mradi huu ni hatua muhimu katika kuboresha hali ya afya ya wananchi na kupambana na changamoto za mazingira zinazotokana na matumizi ya nishati chafu.
ZINAZOFANANA
Samia atambuliwa miongoni mwa Wanawake 100 wenye nguvu zaidi Duniani na Forbes
TMA yatoa tahadhari uwepo wa kimbunga Chido
Kesi ya Waislam kuipinga Bakwata kuanza kusikilzwa mapingamizi mwakani