December 14, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanachuo 2,665 CBE wahitimu ngazi mbalimbali kampasi ya Dar

 

SERIKALI imeahidi kuendelea kukiwezesha Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), ili kiwe chuo bora kituo cha umahiri kwa nchi za Afrika Mashariki na kati na kusini mwa Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, wakati wa mahafali ya 59 ya chuo cha elimu ya biashata ambapo wahitimu 2,665 walitunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali.

Alisema serikali inajivunia kua na chuo hicho ambacho kimekuwa mahiri kwa kutoa wanataaluma wanaotegemwa na viwanda na kampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na chuo hiki ni ishara tosha ya namna chuo hiki kilivyo kimbilio kwa wananchi wengi, tutaendeleza ubora wa elimu inayotolewa hapa tunataka iwe elimu ya vitendo iwawezeshe wahitimu waajiriwe na waweze kujiajiri,” alisema

Alisema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya chuo hicho yakiwemo majengo ya mihadhara na madarasa ili kuongeza kiwango cha wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka.

Kigahe alisema maboresho hayo yote yatafanyika kwenye kampasi zote za chuo hicho ambazo ziko kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Dodoma.

“Lengo ni kuona elimu inayotolewa na chuo hiki inapatokana kwenye mikoa mbalimbali na hata Zanzibar kwa hiyo kila mwaka tutaendelea kutoa fedha za kukiendeleza na tutapenda kuona wanaohitimu hapa wanakuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe,” alisema

Alisema serikali inaagiza tafiti mbalimbali zinazofanywa na CBE ziende kuwasaidia wajasiriamali kwani inaonekana vijana wengi hawana uthubutu kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

“Vijana wengi hawana ujasiri wakufanya biashara na ujasiriamali kwa hiyo tafiti ziwasaidie vijana kwa hiyo tunataka elimu itoke kwenye nadharia iende kwenye vitendo ili ikachangamshe biashara za nchi hii,” alisema

Mkuu wa chuo cha CBE, Profesa Edda Lwoga, alisema chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1965 kimekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake kwa kuwa na wahitimu wengi ambao wako serikalini na sekta binafsi.

Alisema kwa muda wote huo CBE inajivunia kuweza kuzalisha idadi kubwa ya wataalamu wa biashara na wataalamu ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kwenye uchumi.

Alisema chuo kimetekeleza majuku yake ya msingi kama kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye sekta ya biashara, metrolojia na viwanda na kwamba miaka kimepiga hatua kubwa sana kwenye kufanya tafiti mbalimbali.

“Tulianza na wanafunzi wachache sana lakini sasa tuna wanafunzi zaidi ya 20,000 kwenye kampasi zetu nne lakini kutokana na umuhimu wa elimu ya biashara tuliongeza kampasi Dodoma, Mwanza na nyingine Mbeya kwa hiyo kwa sasa ziko nne,” alisema

Alisema mitaala ya chuo hicho pia imejikita kwenye sekta ya utalii, ununuzi na ugavi, Tehama, vipimo na viwango nan i chuo pekee kinachotoa elimu ya vipimo na viwango kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki.

“ Katika kusogeza huduma yetu ya elimu ili iweze kufika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi, CBE mwaka huu tulianza kutoa shahada za uzamili kwa njia ya mtandao na zimepokelewa vizuri sana na wananchi na mpaka sasa tumetoa shahada hizo nane,” alisema Profesa Lwoga.

Alisema wanatoa Shahada za Uzamili kwenye eneo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), usimamizi wa miradi na biashara za kimataifa usimamizi wa fedha na biashara.

“Katika kuboresha mitaala yetu mwaka 2021 tulizindua mwongozo wa atamizi za biashara ambapo wanafunzi wanasajii bunifu zao za biashara tunazisajili tunawaendeleza wanafanya baishara wakiwa chuoni mpaka sasa vijana zaidi ya 412 wanaendelea na biashara kupitia mfumo huo,” alisema.

About The Author

error: Content is protected !!