WAJUMBE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtaa wa Chinyoya Kata ya Kilimani Wilaya ya Dodoma Mjini, Jijini Dodoma wamemkata Mgombea aliyeteuliwa na chama hicho kuwania nafasi ya uwenyekiti wakidai mgombea huyo amekuwa akijifanya Mungu mtu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimani, Dodoma … (endelea).
Wajumbe hao wametoa malalamiko yao wakati wakizungumza na waandishi wa habari Mtaani hapo huku wakidai kuwa mgombea aliyeteuliwa kugombea nafasi hiyo amekuwa akifanya maamuzi kwa matakwa yake binafsi nakutumia ubabe katika kuwaongoza.
Aidha wameongeza kuwa mwenyekiti huyo aliyeteuliwa na CCM kuwania nafsi hiyo amekuwa akichangia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi kwa wananchi huku wakikiambia CCM imekuwa ikifanya hivyo kutokujua nakudai maamuzi ya chama chao yamekuwa yakiwaumiza wananchi.
Siku za hivi karibu katika Mkoa wa Dodoma yameibuka malalamiko kadhaa ya baadhi ya watia nia wa nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za mitaa kuchanguliwa na wajumbe lakini majina yao yakishaenda ngazi ya juu ya uteuzi yamekuwa hayarudishwi nakudai kuteulia kwa wagombea ambao hawajachanguliwa na wajumbe.
Miongoni mwa wilaya zilitoa malalamiko kuhusu uteuzi wa wagombea wa chama hicho kuwa na dosari ni pamoja na Dodoma Mjini, Mpwapwa na Chemba.
Akijibu malalamiko hayo Katibu wa Itikati na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed amesema chama hicho kimekuwa kikiteuwa wagombea ambao wanauzika nakunukia kwa watu na siyo wanaonuka kwa watu.
Amesema kuwa kura za maoni zinabaki kuwa kura za maoni nahatakama akishinda hazimpi ‘turufi’ ya kuteulia kuwania nafsi za uongozi nakuongeza ili mgombea wa chama hicho ateuliwa kupeperusha bendera ni lazima awe amesalimika na makosa aliyoyafanya na akikutwa nayo hata kama amefanya vizuri hawezi kuteulia.
ZINAZOFANANA
Prof. Kitila: Lissu ameudanganya Umma, hatukupanga mapinduzi
TMA yatoa tahadhari uwepo wa kimbunga Chido
Lissu ataka Chadema mpya kwenye uongozi wake