MAHAKAMA ya Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, jana imemhukumu kifungo cha miaka 60 jela afisa mtendaji wa kijiji cha Paramawe, Richard Kiwela (45), kwa makosa matatu, ikiwemo kuibia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kiasi cha Sh. 2,881,000 alizokusanya kupitia mashine ya POS. Anaripoti Ibrahim Yassin, Nkasi, Rukwa … (endelea).
Mtuhumiwa alikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na kuisababishia hasara mamlaka, kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 pamoja na sheria ya uhujum u uchumi. Mashtaka yalitolewa na mwendes ha mashitaka wa TAKUKURU, Mzalendo Widege.
Mahakama ilipokea vielelezo 12 vilivyowasilishwa na upande wa mashtaka, ambavyo mtuhumiwa alikubali, hivyo kuimarisha kesi dhidi yake. Mwendesha mashitaka alieleza kuwa Kiwela alikabidhiwa mashine hiyo mnamo Novemba 11, 2018, na alikusanya jumla ya Sh. 55,825,600, lakini alishindwa kuwasilisha kiasi cha Sh. 2,881,000.
Hakimu mkazi mfawidhi, Denis Luwungo, alikubaliana na mashitaka hayo, akisema kuwa mtuhumiwa amekiri makosa yake. Kila kosa lilipewa adhabu ya miaka 20, ambapo mtuhumiwa ataitumikia kifungo hicho kwa pamoja. Ingawa ni kosa lake la kwanza, hakimu alisisitiza kuwa adhabu hiyo ni muhimu ili kuwa fundisho kwa watumishi wengine wa umma.
Kiwela aliiomba mahakama isimpatie adhabu kali, akidai kuwa yuko tayari kurejesha fedha hizo endapo mwajiri wake atamlipa. Upande wa mashitaka ulisisitiza umuhimu wa adhabu kubwa ili kuzuia uhalifu wa aina hiyo katika serikali.
Hata hivyo rufaa ipo wazi kwa siku 30 kwa mtuhumiwa endapo hataridhika na hukumu hiyo.
Nje ya mahakama baadhi ya wananchi waliokuwepo mahakamani hapo walitoa mawazo tofauti kulingana na ukubwa wa adhabu huku wengine wakisema adhabu ipo sahihi kutokana na vifungu vilivyotajwa.
ZINAZOFANANA
Wakazi wa Mdundwaro waishukuru TASAF kuwajengea nyumba ya watumishi
Tanzania yakosa Bil 9.3 za nyama
Tanzania yang’ara Uimara wa kiuchumi: IMF yathibitisha Tanzania kuimalika