MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwafikia wateja wake katika maeneo mbalimbali ya kihuduma katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani ili wanatatua na kuboresha huduma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja DAWASA, CPA (T), Rithamary Lwabulinda ameeleza kuwa kwa kipindi chote cha maadhimisho Watumishi wa Mamlaka watakuwa katika mitaani kusikiliza, kupokea na kutatua changamoto mbalimbali za kihuduma zinazowakabili ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora.
“Wiki hii ni muhimu sana katika usimamizi wa utoaji huduma kwani itasaidia kuimarisha mahusiano baina ya Mamlaka na wateja wake, lakini zaidi kuwafikia Wananchi katika makazi yao na kupata majibu, maoni na mapendekezo yanayosaidia kuboresha huduma yetu” ameeleza Lwabulinda.
Kwa upande wake, ndugu Hashim Ally mkazi wa Kisarawe ameipongeza DAWASA kwa kufika mtaani na kuwasikiliza kwani itasaidia kuboresha huduma na kuchagiza mahusiano chanya kati ya wateja na Taasisi.
Wiki ya huduma imebeba kauli mbiu isemayo “Ni zaidi ya matarajio” huadhimishwa tarehe 7 – 11 mwezi Oktoba kila Mwaka.
ZINAZOFANANA
Serikali yaipa ITA jukumu la utafiti wa mapato
Benki ya NBC yatambulisha kampeni ya Kilimo Mahususi kwa wakulima na wafugaji Mbeya
Upelelezi wakwamisha kesi ya Boni Yai