November 12, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Boni Yai aruka kihunzi, asema ameshuhudia mengi gerezani

 

BAADA ya kusota gerezani siku 19 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob ‘Boni Yai’ hatimaye amepata dhamana. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 7 Oktoba, 2024 Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga ametupilia mbali pingamizi la upande wa Jamhuri waliliwasilishwa mahakamani hapo kupinga Boni Yai asipewe dhamana kwa kile walichodai kuwa wanahofia usalama wake akiwa uraiani.

Kupitia kiapo kilichowasalishwa mahakamani hapo na upande Jamhuri cha Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni (RCO), Davis Msangi kilichozuia dhamana ya ‘Boni’ kwa kudai kuwa alimtaarifu kuwa akibaki uraiani hatakuwa salama kwa kuwa kina kitisho cha kutekwa au kuuawa.

Kiapo hiki kilipinga na Wakili wa Utetezi Peter Kibatala na hatimaye leo Hakimu Kiswaga amenukuu ibara ya 13 (6a&b) na Kifungu cha 148 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jina kinatoa mazingira kwa mahakama ya kutoa au kutotoa dhamana.

“Sababu zilizotolewa hazina maelezo ya ziada ya kwanini mahakama isitoe dhamana. Iwapo mjibu maombi ametoa maelezo juu ya usalama wake nilitegemea muombaji (Jamhuri) ataleta uthibitisho juu ya maelezo ya Mjibu maombi.

“Pamoja na kwamba upande wa majibu maombi haujaleta kiapo kinzani lakini kiapo cha muombaji haitoshi mahakama kumnyima dhamana mtuhumiwa ukizingatia hii ni haki ya kikatiba,” anasema Hakimu Kiswaga

Hakimu Kiswaga amesema kuwa mahakama hiyo haikubali maombi ya Jamhuri hivyo basi mjibu maombi (Boni), atapewa dhamana kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na mahakama hii.

Serikali yataka Boni anyang’anywe hati ya Kusafiria

Baada ya uamuzi huo wakili wa Serikili, Job Mrema aliwasilisha mahakama hapo maombi ya masharti ya dhamana.

Upande wa Jamhuri umekitaja kifungu cha 148 (6) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kitumike kumpa dhamana mshtakiwa kwa masharti ya kunyang’anywa hati ya kusafiri pamoja na kuzuiliwa kutoka nje ya Dar es Salaam.

kuhusiana na masharti ya lazima ya masharti ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Mashariti ya lazima ni pamoja na kukabidhi hati ya kusafiria pamoja na kuzuia nyendo za mshtakiwa kutoka maeneo anayoishi. Ukienda kusoma kifungu cha 7 inasisitiza masharti ta sita ni ya lazima ni ombi letu tunaiomba mahakama izingatie kifungu hiko. Kifingi kidogo cha saba kinaipa Mamlaka Mahakama ya hili.

Kifungu kidogo cha saba (c) sharti la ziada inatoa zuio la mshaktakiwa kutokutenda kosa lolote la jinai kwa sababu shauri hili limezaliwa kwenye shauri 1185/ 2024 tuhuma zinazomkabili mshtakiwa . boniface akiachwa hivi hivi tabia hii itaendelea . Hoja yetu tunaomba azuiliwe . Pili katika kueleza kifungu cha 148 Boniface asiruhusiwe kutoka jijini Dar es Salaam.

Wakili Kibatala ameieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa ni kiongozi ambaye aliwahi kuwa Meya wa Manispaa mbili ya Kinondoni na ile ya Ubungo na sasa kiongozi hivyo anaweza kujidhamini mwenyewe.

Hakimu Kiswaga amesema kuwa Boniface atadhaminiwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka ofisi ya serikali za mitaa na watasiini bondi kiasi cha Sh. 7 milioni huku akitakiwa asisafiri kweda nje ya nchi bila kuitaarifu mahakama.

Nje ya Mahakama
Wafuasi wa Chadema wakionekana wanafuraha walijikusanya nje ya mahakama na kujihamasisha wakutane kwenye Ofisi za Chadema Kanda ya Pwani zilizopo Kinondoni mtaa wa Ufipa.

Boni asema neno
Boni Yai akizungumza baada ya kuachiwa kwa dhamana amasema kuwa siku 19 alizokaa kwenye mahabusu ya gareza la Segerea alijionea mengi huku akisema ukiitaka kuifahamu nchi tembele ukitaka kuijua nchi nenda jela “kuna mambo makubwa nimejifunza kuwa kwangu kule kumekuwa kama darasa nimekutana na watu wengi mambo kadhaa nimeyafahamu nimeona niwalipie watuhimiwa 20 gharama za uwakilishi mahakamani ”

Boni amesema kuwa atawalipia wafungwa 10 waliotakuwa walipe faini ili watoke gerezani tayari mmoja ameshamlipia.

Boni amesema kuwa hakukamatwa na kwamba ataelezea Watanzania mkasa wote siku akipata nafasi “nilipelekwa Polisi nikiwa na boksa ‘(nguo ya ndani) nitaeleza yote.

About The Author