WAZIRI wa mambo ya nje wa Israel amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) António Guterres ”Hana ruhusa” kuingia Israel na amepigwa marufuku nchini humo.
Israel Katz anasema uamuzi wake unafuatia hatua ya Guterres “kutolaani” shambulio la kombora la Iran dhidi ya Israel siku ya Jumanne.
Anamshutumu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kwa kuwa “mpinzani wa Israel” na kutoa “msaada kwa magaidi, wabakaji na wauaji.Guterres atakumbukwa kama doa katika historia ya Umoja wa Mataifa kwa vizazi vijavyo.”
Jana, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alilaani “kuongezeka kwa mzozo wa Mashariki ya Kati” na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.
ZINAZOFANANA
Waziri Mkuu wa Canada kujiuzulu?
Maafisa Korea Kusini wajaribu kumkamata Rais Yoon
Morocco kuwapa wanawake haki zaidi