WANANACHI wa Kijiji cha Ngombo katiika Kata ya Biro wilayani Malinyi mkoa wa Morogoro wameiomba serikali kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka kuwahamisha katika kijiji chao cha asili ambacho wamekuwepo hapo kwa zaidi ya karne tatu baada ya kuambiwa ni wavamizi wa eneo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam na mjini Malinyi hivi karibuni, wawakilishi wa kijiji hicho wamesema wao wapo hapo kwa muda mrefu kuanzia mababu na kwamba wanashangaa kuambiwa wahame na Mamlaka ya Hifadhi kwa madai ya uharibifu wa vyanzo vya maji.
“Tunamwomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati suala hili kwani ni kutunyanyasa kwenye eneo letu la asili. Kumekuwa na kuwa mamlaka zinazosimamia maeneo ya hifadhi kutaka wanakijiji katika eneo hilo kuondoka haraka,” alisema Ananias Patitu.
Amesema wananchi wa Kijiji hicho hawapo tayari kuhama na kwamba watafanya kila liwezekanavyo kumfikishia Rais Samia ujumbe wao na kumwomba awasaidie wasihamishwe kwenye Kijiji chao cha asili.
Alielezea wasiwasi na hofu kubwa imetawala miongoni mwa wanakijiji na kuiomba serikali isaidie wasiondolewe katika maeneo yao asili kwa sababu hawajui wapi wataishi ikiwa wataondolewa.
“Tunaiomba serikali ituonea huruma na kutuacha tuendelee kuishi hapa kwani tupo tangu miaka mingi sana na tumerithi kijii hiki kutoka kwa mababu zetu ambao nao walirithi kwa mababu zao zaidi ya karne tatu,” alisema Patitu.
Alisema kuwa kumekuwa na madai ya kuharibu chanzo cha maji cha bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Hydro-electric Power) kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji wakati wanakijiji wakieleza kuwa wanaelewa umuhimu wa vyanzo vya maji na hakuna uharibifu wowote uliofanyika mpaka sasa.
Naye mwakilishi mwingine wa Kijiji hicho, Davidi Mkumba alisema kwa muda wote ambao wameishi kijijini hapo wamewekeza vya kutosha na kijiji chao kimekuwa miongoni mwa vijiji vinavyochangia pato kwa serikali .
“Hiki kijiji chetu kimesajiliwa na tumefanikiwa kujenga huduma zote muhimu za kijamii kama vile shule na kituo cha huduma ya afya,” alisema Mkumba Mkumba na kuongoza kuondelewa kwa wananchi kijijini hapo itakuwa ni uonevu.
Kupitia vyombo vya habari, Mkumba amesema wameambiwa kuwa ndani ya miezi miwili wawe wamekwisha ondoka eneo hilo ili kuipisha seriakli iendelee kutunza eneo hilo kwa manufaa makubwa ya nchi.
Juhudi zaidi zinaendelea kuwafikia viongozi wa Halmashauri ya Malinyi ili watoe ufafanuzi zaidi kuhusu hilo.
ZINAZOFANANA
TRA yazindua ofisi ya walipa kodi binafsi
Mwenge wa uhuru wazindua mradi wa maji Kahangara -Magu
DC: Ilala hali ni shwari uandikishaji