SAA chache baada ya kusambaa kwa taarifa za kukamatwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, Jeshi la Polisi limethibitisha kumshikilia kwa tuhuma za kijinai. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa fupi ya msemaji wa Jeshi hilo, David Misime, kwa umma imesema kada huyo hajatekwa bali amekamatwa na polisi.
“Jeshi la Polisi limemkamata na linamshikilia Boniface Jacob, mkazi wa Mbezi kwa Msakuzi jijini Dar es Salaam kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo. Wananchi wapuuze uongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa,” amesema Misime.
Taarifa zinaeleza kuwa Jacob alikamatwa maeneo ya Sinza jioni ya leo -tarehe 18 Septemba, na kupelekwa kituo cha polisi Oysterbay
ZINAZOFANANA
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema