Milio ya risasi imesikika katika mji mkuu wa Mali, Bamako na kusababisha ripoti kwamba kambi moja ya usalama imeshambuliwa. Inaripoti BBC, Bamako, Mali
Video kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi ukipaa kutoka sehemu ya jiji, huku baadhi wakieleza kuwa moshi huo huenda unatoka katika kituo cha polisi au cha kijeshi.
Vyanzo vya usalama viliambia vyombo vya habari vya Ufaransa RFI na AFP kwamba watu wenye silaha walishambulia kambi moja au zaidi katika mji huo mkuu.
Mali ni mojawapo ya nchi za Afrika Magharibi ambazo zimekuwa zikipambana na waasi wa Kiislamu kwa zaidi ya muongo mmoja. Hata hivyo, katika tukio la sasa haijulikani ni nani aliyehusika na ufyatuaji huo wa risasi.
Jeshi lilitwaa mamlaka katika mapinduzi mwaka wa 2021 na kuishutumu serikali kwa kushindwa kufanya vya kutosha kuzima uasi huo.
Hata hivyo, miaka mitatu baadaye, hakuna dalili ya mashambulizi kumalizika.
Walioshuhudia waliambia shirika la habari la Reuters kwamba milio ya risasi ilianza majira ya saa 05:30 alfajiri.
Watu waliokuwa wakielekea msikitini kwa ajili ya swala ya asubuhi walirejea majumbani huku milio ya risasi ikivuma, Reuters ilisema.
ZINAZOFANANA
Putin, Pezeshkian waahidi kuimarisha uhusiano
Gachagua kunyoa au kusuka Bunge la Seneti wiki ijayo
Watu 78 wafariki baada ya boti kuzama Kongo, 58 waokolewa