MGOMBEA urais wa chama cha Republican, Donald Trump, yuko salama baada ya kile FBI ilisema inaonekana ni jaribio la mauaji Jumapili alipokuwa akicheza gofu kwenye uwanja wake wa West Palm Beach, Florida. FLORIDA, Marekani
Maafisa wa usalama wamesema maafisa wa idara ya ulinzi wa viongozi ya Marekani walimwona na kumfyatulia risasi mtu aliyekuwa na bunduki katika baadhi ya vichaka karibu na eneo hilo akiwa na bunduki aina ya AK-47.
Vyombo vya habari, vikiwemo The Associated Press, The New York Times na Fox News Channel, vilimtaja mshukiwa huyo kuwa ni Ryan Wesley Routh, 58, wa Hawaii, vikiwanukuu maafisa wa sheria ambao hawakutajwa majina
ZINAZOFANANA
Putin, Pezeshkian waahidi kuimarisha uhusiano
Gachagua kunyoa au kusuka Bunge la Seneti wiki ijayo
Watu 78 wafariki baada ya boti kuzama Kongo, 58 waokolewa