UONGOZI wa Kanisa la Mlima wa Nuru Assembless of God (CAG) lililopo Chamelo Nzuguni “B”Jijini Dodoma limekea vikali vitendo nchini vya utekaji na watu kupotea na kukutwa wamekufa bila sababu na kwa minajiri hiyo kanisa limeanzisha maobi rasm ya kuliombea taifa na viongozi ili taifa liwe na amani na utulivu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Uongozi huo kanisa la mahali pamoja la CAG Chamelo,Nzuguni “B”Jijini Dodoma umesema maombi hayo yanalenga zaidi kuliombea taifa,vyombo vya ulinzi na usalama,muhimili wa Bunge,Mahakama,Serikali kuu,Rais wa Jamhuri ya Tanzania,Baraza la Mawaziri pamoja na tume ya Uchaguzi.
Leo Jumapili Septemba 15 Mwaka huu Mmoja wa kiongozi ndani ya kanisa hilo ambaye ni Katibu wa kanisa la mahali pamoja CAG Mlima wa Nuru Dk. Musa Halinginoti,akisoma matangazo muda mfupi kabla ya mahubiri amesema kuwa kutokana na matukio yanayoendelea ya utekaji,watu kupotea, kuuliwa na vitendo vya ukatili vinavyoendelea kanisa linachukizwa na matukio hayo hivyo ni wajibu wa kila muhumini kuliombea taifa ili matukio hayo yakome na yasijirudie tena.
“Kila muunini wa kanisa hili akazane kuliombea taifa ili Mungu azuie vitendo viovu vinavyoendelea kwani kwa matukio hayo ni machukizo mbele za Mungu na njia pekee ta kukomesha matukio hayo ni kufanya maombi.
“Tunaelekea katika uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa na baadaye uchaguzi Mkuu wa 2025,lakini kwa sasa tunashuhudia matukio mbalimbali ya kutisha takitokea jambo ambalo siyo zuri kwa taifa letu ambalo linahesabika kama taifa la kuigwa kwa kuwa na utulivu na amani.
“Sisi hatukuzaliwa kuwa kama mataifa ambayo yamezoea kuwa na vurugu sisi taifa letu ni kitovu cha amani ,upendo na utulivu mkubwa hivyo ni jukumu la kila mtu ambaye anamwamini Mungu kuomba kwa juhudi kwa ajili ya ulinzi wa nguvu ya Mungu ili taifa liendelee kuwa na amani” amesem Dk.Halinginoti.
Kuhusu suala la mambo ya siasa amesema wanasiasa wanatakiwa kutambua kuwa Tanzania ni nchi ya amani hivyo wanasiasa wanatakiwa kuendesha siasa zenye utulivu,amani na upendo na zisizokuwa na vurugu ambazo zinaweza kusababisha kupasuka kwa taifa kutokana na vurugu.
“Wanasiasa wanatakiwa kutambua kuwa wao ni muhimu sana katika kutunza tunu ya taifa kwa kulinda amani ya nchi hivyo wanatakiwa kufanya siasa ambazo si za ubinafsi,wala upendeleo wa aina yoyote unaoweza kuchafua hali ya hewa,” ameeleza Dk.Halinginoti.
ZINAZOFANANA
Polisi: Waharifu 2024 wapungua mkoani Songwe
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Mil.600 zatengwa kupeleka umeme Kijiji cha Ijinga – Magu