
Ian Khama
RAIS wa zamani wa Botswana, Ian Khama amerejea nchini bila kutarajiwa baada ya miaka mitatu ya kukaa uhamishoni, na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yakiwemo ya kutakatisha fedha na kumiliki silaha kinyume cha sheria. GABORONE, Botswana.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 71 alikuwa amedai hivi majuzi kulikuwa na njama ya kumtilia sumu ikiwa angekanyaga nyumbani kwake.
Serikali ilizitaja tuhuma hizo kuwa za “kuudhi”.
Wafuasi wake waliimba “Jenerali amerejea” wakati Khama akiondoka kwenye mahakama siku ya Ijumaa katika mji mkuu, Gaborone
ZINAZOFANANA
Kadinali Robert Prevost atangazwa kuwa Papa mpya
Bunge la Ulaya laitaka Tanzania kumuachia huru Lissu
Waziri Mkuu wa Romania ajiuzulu