JESHI la Polisi Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika tarehe 23 Septemba, 2024 na Chama cha Demokrasia na Maemdeleo (CHADEMA). Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime amesema kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii walisikia viongozi wa Chadema wakihamasisha wananchi wa jiji la Dar es Salaam kuingia barabarani pamoja na kuwalika wakazi ya mikoa mbalimbali kuja kuwaunga mkono.
Amesema mara kadhaa viongozi na wafuasi wa chama hicho wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali yenye lengo la kuleta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi kwa wasababu wanazozijua wao wenyewe.
Misime amesema kutokana na taarifa hiyo Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa viongozi wa chama hicho kuacha kuhamasisha wananchi katika uhalifu huo na yoyote atakayeingia barabarani atakabiriwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za nchi.
Pia ametoa rai kwa wananchu wapenda amani kutokubali kurubuniwa, kudanganywa au kushawishiwa kwa namna yeyote na badala yake waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
ZINAZOFANANA
Polisi wadai Chadema wamewapiga mawe
Serikali yaipa ITA jukumu la utafiti wa mapato
Mbowe, Sugu wakamatwa na Polisi mkoani Songwe