Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ndege aina ya Boeing B787-8 Dreamliner, ambayo ilitarajiwa kutua kwa mara ya kwanza kwa uzinduzi leo tarehe 19 Agosti 2024, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar, haitoweza kufika kama ilivyopangwa kutokana na changamoto za hali ya hewa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar… (endelea).
Mapokezi na sherehe za uzinduzi wa ndege hiyo mpya yalipangwa kufanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi katika uwanja huo wa ndege Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Kaimu mSEMAJI WA serikali, Zanzibar, Raqey Mohamed imesema ratiba mpya ya kuwasili kwa ndege mpya aina ya Boeing B787-8 Dreamliner itatolewa mapcma baada ya kukamilika.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza,” imesema taarifa hiyo.
ZINAZOFANANA
Polisi: Waharifu 2024 wapungua mkoani Songwe
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Mil.600 zatengwa kupeleka umeme Kijiji cha Ijinga – Magu