October 16, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Manchester United kuifungua EPL leo

 

KLABU ya Manchester United itafungua msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza leo ambapo wataikaribisha klabu ya Fulham katika dimba la Old Trafford katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo pendwa zaidi duniani.

Baada ya kua na msimu ambao sio wa kuvutia kwa klabu hiyo msimu huu wanaonekana kuhitaji kurekebisha makosa ambayo waliyafanya msimu uliomalizika, Hii inatokana na sajili ambazo wamezifanya msimu huu na kipimo cha kwanza kitakua kwa vijana kutoka London klabu ya Fulham.

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

Mchezo wa leo unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa kwani klabu ya Fulham pia ni moja ya timu ambazo zimekua na ubora kwenye ligi kuu ya Uingereza, Wakiwa wameongeza wachezaji wenye ubora kwenye kikosi msimu huu.

Ikumbukwe mara ya mwisho klabu ya Fulham kufika katika dimba la Old Trafford walifanikiwa kushinda kwa mabao mawili kwa moja, Hivo mchezo wa leo sio mwepesi kutokana na kilichofanywa mara ya mwisho na Fulham walipokutana tena katika uwanja wao wa nyumbani.

About The Author