KAMATI ya Sheria na hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imemaliza utata kwenye Sakata la usajili la mchezaji Awesu Ali Awesu na kueleza kuwa mchezaji huyo ni mali halali ya klabu ya KMC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Uamuzi wa kamati hiyo umekuja kufuatia klabu ya KMC ambayo inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, kulalamika kutofuatwa kwa utaratibu na klabu ya Simba kwenye usajili wa mchezaji huyo ambaye walikuwa na mkataba nae.
Kwenye kikao chake cha tarehe 10 Agosti 2024, kamati hiyo ilisikiliza pande zote mbili, na kuamua kuwa mchezaji huyo ni mali halali ya KMC na kama Simba wanamuhitaji wanatakiwa kufuata taratibu za klabu hiyo.
Mpaka malalamiko hayo yanafika kwenye kamati hiyo tayari klabu ya Simba ilishamtangaza Awesu kama mchezaji wao mpya, kupitia kurasa mbalimbali za mitandao yao ya kijamii, kisha kuelekea nchini Misri ambapo klabu hiyo iliweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu mpya unaonza tarehe 16 Agosti 2024.
Kabla ya usajili wa mchezaji huyo kufanyika, kmc walishaweka wazi kiasi cha fedha wanachokihitaji ambacho ni shilingi Milioni 200 kwa klabu yoyote inayohitaji huduma ya mchezaji huyo, ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.
ZINAZOFANANA
ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1,000 yapo hapa
Jumapili ya kuchuma na Meridianbet ni leo
Meridianbet yagawa mipira kwa Sinza Star FC