October 16, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Meridianbet yatoa msaada Mbezi

 

Kama ilivyo kawaida kampuni ya Meridianbet leo wamefika eneo la Mbezi jiji Dar-e-salaam na kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwenye eneo hilo.

Meridianbet wamekua wakifanya utaratibu huu kwa miaka mingi wakijitahidi kugawana na jamii yake ambacho wamekivuna, Ambapo leo ni wakazi wa Mbezi wamenufaika ambapo wameweza kupatiwa mipira kadhaa ambayo itaweza kuimarisha ari na hamasi ya mpira wa miguu katika aeneo hilo.

Kama ambavyo inatambulika serikali inajitahidi kuhakikisha inainua sekta ya michezo kwakua ni moja ya sekta ambazo zimekua zikitoa ajira kwa vijana, Hivo Meridianbet wameamua kuinga mkono serikali kwa kuhakikisha nao watoa ushirikiano katika kukuza michezo nchini na ndio sababu wametoa msaada wa mipira leo katika eneo la Mbezi.

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi Nancy Ingram alikua mbele kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na kusema “Nina furaha kubwa kuwepo mahali hapa leo na kama mnavyojua michezo imekua moja ya sekta muhimu kwa vijana kupata ajira siku hizi, Hivo sisi tumeamua kuhakikisha tunawashika mkono vijana wa eneo hili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao katika suala zima la michezo haswa mpira wa miguu”

Aidha Diwani wa Jimbo la Mbezi ya Juu Mheshimiwa Anna Lukindo alikuwepo katika zoezi hilo bila kusita alizungumza machache “ Kiukweli niwashukuru sana Meridianbet kwa kufika hapa leo na kuweza kutoa msaada wa vifaa vya michezo ambavyo vitawasaidia vijana wetu wanaopenda michezo kufikia malengo yao, Lakini pia nipende kutoa rai kwa makampuni mengine wanaweza kuiga haya mazuri ambayo yanafanywa na Meridianbet kuhakikisha wanaisaidia jamii yao”

About The Author