September 18, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Makonda arejea, akagua uwanja wa ndege Kisongo

 

BAADA ya ukimya wa zaidi ya siku 33, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amerejea katika kituo chake cha kazi leo tarehe 16 Agosti na kumaliza minong’ono iliyokuwa imeenea mitaani juu ya alipo kiongozi huyo machachari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Makonda ambaye anafuatiliwa na Watanzania wengi kutokana na matendo na utendaji wake wenye utata, hapo awali iliripotiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu kwamba amekwenda likizo na kukaimisha majukumu yake kwake.

Hata hivyo, minong’ono ilizidi zaidi baada ya watu kuhoji uhalali wa likizo hiyo hasa ikizingatiwa alianza kuitumia nafasi hiyo ya mkuu wa mkoa tarehe 31 Machi mwaka huu, muda ambao kwa taratibu za likizo serikalini, hakuwa ametimiza muda wa miezi nane kazini.

Ukimya wake ulizidi kuibua mjadala huku baadhi ya watu wakihoji kuhusu afya yake baada ya kuibuka madai katika mitandao ya kijamii kwamba yupo nje ya nchi anatibiwa baada kunywesha sumu jambo ambalo hata hivyo hakuna kiongozi wa serikali aliyewahi kulizungumzia.

Leo Ijumaa mkuu huyo wa mkoa wa Arusha, amemaliza minong’ono hiyo baada ya kutua mkoani humo na kufanya ukaguzi wa jengo jipya la Uwanja wa ndege wa Kisongo jijini Arusha.

About The Author