November 24, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais awataka mawaziri wajiongeze

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka mawaziri na watendaji wengine anaowateua kwenye nyadhifa mbalimbali wajionge pindi wanapokutana na suala lisilohusu taaluma wasizozisomea. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…. (endelea).

Rais Samia ameyasema maagizo hayo leo tarehe 15 Agosti 2024, wakati anawaapisha mawaziri na watendaji wapya wa serikali aliowateua jana tarehe 14 Agosti 2024.

Rais Samia amewataka mawaziri hao waende wakafanye kazi na wanapoona kuna suala mbele yao halipo kwenye taaluma tofauti basi wajiongeze.

“Nachotaka kusema ni kile alichokisema Makamu wa Rais, (Dk. Philip Mpango) kwamba kwenye kufanya kazi zenu kuna professionalism utaalamu wako uliosomea binafsi lakini kuna kujiongeza kutumia common sense (ufahamu) yako kwa hiyo pale mnapoona inaweza kutumika vizuri common sense mjiongeze mfanye kazi tuwatumike wananchi.”

Ametanabaisha kuwa asingeweza kutumia muda mrefu kuzungumza kwa kuwa anahudhuria kikao cha Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mawaziri walioapishwa leo ni pamoja na William Lukuvi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Prof. Paramagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Wengine ni Jenista Mhagama ambaye ameapishwa kuwa Waziri wa Afya na kuchukua nafasi ya Ummy Mwalimu ambaye hajapangiwa kazi nyingine.
Balozi Dk. Pindi Hazara Chana ameapishwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Balozi Pindi anachukua
nafasi ya Angellah Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.

About The Author