November 24, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Samia afagia ofisi ya AG, Hamza amrithi Feleshi

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ikiwemo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Jaji wa Mahakama ya Rufani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Hamza Johari ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkutu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huu, Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), anachukua nafasi ya Jaji Dk. Eliezer Feleshi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani;

Taarifa hiyo imesema Sarnwel Maneno ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Maneno alikuwa Msaidizi wa Rais, Sheria. Maneno anachukua nafasi ya Balozi Prof. Kennedy Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Sheria na Mikataba.

Pia Samia amemteua Dk. Ally Saleh Possi kuwa Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Dk. Possi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.

About The Author