
Msemaji wa Polisi, DCP David Misime
JESHI la Polisi limesema halijapiga marufuku kufanyika mikutano ya nje ya hadhara na ile ya ndani ili mradi inafuata matakwa ya sheria za nchi. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Agosti 2024 na Msemaji wa Jeshi hilo nchini, DCP – David Misime, killichopigwa marufuku ni mkusanyiko uliokuwa umeitishwa na Viongozi wa Chadema huko Jijini Mbeya kwa kivuli cha kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani.
Hayo yanajiri wakati Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) likiwa limeratibu kongamano la maadhimisho ya siku ya vijana duniani lililotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Maadhimisho hayo ambayo yalikuwa yafanyike leo Jumatatu, mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
ZINAZOFANANA
Uingereza yafurahishwa na maboresho Bandari ya Dar, yaipongeza serikali
Vyombo vya dola kikwazo kwa mawakili kutimiza majukumu yao
Mkuu wa mkoa Mwanza aitisha kikao kumsaka kada wa Chadema