December 22, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

M23 wateka mji wa mpakani na Uganda

 

Waasi wa M23 wamedaiwa kuuteka mji mmoja wa mpakani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bila mapigano jana Jumapili siku ambayo usitishaji mapigano kati ya DRC na nchi jirani ya Rwanda ulikusudiwa kuanza kutekelezwa. Inaripotiwa Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mji wa Ishasha uliopo mpakani na Uganda, umekuwa wa karibuni zaidi kuangukia mikononi mwa kundi hilo linaloungwa mkono na Rwanda.

M23 imeteka maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo toka ilipoanzisha mashambulizi yake mwishoni mwa 2021.

Kiongozi wa mashirika ya kiraia Romy Sawasawa amelieleza Shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa Ishasha imechukuliwa bila upinzani na kuwa chini ya udhibiti wa M23.

Maafisa wa polisi wa Congo walivuka mpaka hadi Uganda wakikimbia waasi waliokuwa wengi na silaha za kutosha.

About The Author

error: Content is protected !!