SHIRIKA la WaterAid limekabidhi mradi wa uboreshaji wa huduma za miondombinu ya maji na usafi wa mazingira Wilaya ya Hanang mkoani Manyara uliogharimu Sh million 425 na unalenga kuwafikia wanufaika wasiopungua 20,036. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkaazi wa shirika hilo, Ana Mzinga, wakati wa halfa ya makabidhiano ya mradi huo katika kijiji cha Bashang na Laghanga vilivyopo katika Wilaya ya Hanang uliokamilika ndani ya mwaka mmoja chini ya ufadhili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.
Mzinga alisema Septemba Mwaka 2023 walifanikiwa kuzindua utekelezaji wa mradi huo mjini Katesh katika kikao cha wadau hatimaye kwa sasa umekamilika na wananchi kuanza kunufaika.
Aidha, alisema katika kikao hicho yapo mengi yaliwasilishwa na kujadiliwa kubwa lililobaki kwao kama taasisi lilikuwa lile la kuahidiwa ushirikiano wa dhati wa kitendaji, ushauri wa kiuongozi na ulinzi katika kutekeleza mradi huu.
“Tunakiri kupata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini na wataalamu wote katika kutekeleza mradi huu na mpaka sasa umefanikiwa kukamilika kwa asilimia 100 kwa taasisi zote tatu zilizolengwa kwa mradi huu ikiwemo miundombinu ya vyoo bora, miundombinu ya usambazaji wa maji safi, miundombinu ya usafi binafsi na usafi wa kitaasisi na uelimishaji wa jamii ya watumiaji wa miundombinu,”alisema.
Mzinga alisema Shirika la WaterAid, ni taasisi isiyo ya kiserikali inayotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na serikali ili kufikia watu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni kwa huduma ya maji safi na salama, vyoo bora na mazingira salama ya usafi na usafi binafsi.
Meneja Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki, Leah Kaguara, alisema WaterAid inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa kila mtu anafikiwa na huduma za maji salama, usafi wa mazingira na usafi.
Alisema WaterAid ilizindua mkakati wake mpya wa kimataifa mwaka 2022 na programu za nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Tanzania zilitengeneza na kuzindua mikakati yao mwaka 2023.
“Lengo letu la kwanza katika mkakati huu kusaidia kupatikana kwa huduma za maji, usafi wa mazingira na usafi (WASH) ziwe endelevu inayojumuisha na salama. huduma katika eneo la Wilaya ya Hanang kwa ajili ya mabadiliko mapana huku lengo la pili likilenga kuweka kipaumbele cha WASH katika sekta ya afya ili kuboresha afya ya umma,”alisema.
Alisema wataendelea kufanya kazi mjini Hanang ili kuunga mkono mipango ya serikali ambayo inalenga kuhakikisha kila mtu katika wilaya hiyo anakuwa na huduma endelevu zinazojumuisha WASH.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang , Athuman Likeyekeye, alishukuru kwa mradi huo na kueleza kuwa miundombinu yote iliyopangwa kutekelezwa imekamilika vizuri na ipo tayari kwa matumizi.
Alisema mradi huo utawanufaisha wananchi wa kata ya Laghanga, Wareta na maeneo ya jirani wakiwemo wanafunzi, wagonjwa.
ZINAZOFANANA
Polisi: Waharifu 2024 wapungua mkoani Songwe
Jeshi la Polisi: Sherekeheni sikukuu kwa utulivu na amani
Mil.600 zatengwa kupeleka umeme Kijiji cha Ijinga – Magu