December 26, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Samia apewa tano mapambano kupunguza vifo kina mama na watoto

 

WANAWAKE wanaojifungua katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, wameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuongea idadi ya hospitali na vituo vya afya hatua iliyosaidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Wakizungumza katika nyakati tofauti, kina mama hao walisema zamani kulikuwa na idadi kubwa ya vifo vya kina mama na watoto sababu wengi walikuwa wanajifungulia nyumbani kutokana na ukosefu wa hospitali maeneo ya karibu.

Fatima Selemani, mkazi wa Kingolwira, alisema hivi sasa majengo ya hospitali nyingi yameboreshwa kitendo kilichopelekea wananchi kuhudumiwa katika mazingira mazuri kama nchi zilizoendelea.

“Namshukuru Rais Samia kwa kutusogezea huduma karibu, hivi sasa tunapata huduma nzuri, vitanda vizuri chooni usiseme ni raha kwa kweli. Rais Samia kweli amefanya kazi,” alisema Fatuma.

Sara Hoseah, kutoka Kijiji cha Bwawani, alisema “tunamshukru Rais Samia ametuboreshea huduma za afya sasa hivi watoto Wetu wanaendelea vizuri. Zamani tulikuwa tunajifungulia nyumbani vito vilikuwa vingi lakini sasa hivi hospitali ni nyingi vimelungua.”

Naye Christina Karoli, mama wa mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati (mtoto njiti), amesema Rais Samia amewaheshimisha wanawake kwa kutekeleza kwa vitendo azma yake ya kuhakikisha wanajifungua watoto salama.

Amesema katika hospitali hiyo kuna vitanda 15 vya watoto njiti, tofauti na ilivyokuwa awali.

About The Author

error: Content is protected !!