September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ujenzi wa bandari ya uvuvi Kilwa wafikiwa 63%, kukamilika Feb 2025

 

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambao mpaka sasa umefikia asilimia 63 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwaka 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Waziri Ulega amesema hayo leo Jumanne alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaofanyika wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

Amesema bandari hiyo ya uvuvi inayojengwa kwa fedha za ndani ni mradi wa kielelezo unaotekelezwa chini ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Mradi huu tuutazame kama mboni ya jicho letu ili uwe endelevu kwa maana ukikamilika utainua uchumi wa Kilwa, ukanda wa Kusini na Taifa kwa ujumla,” amesema.

“Nimefurahi hatua ni nzuri, tumepiga hatua zaidi ya nusu, muhimu kuhakikisha kazi inakwisha kwa wakati ili Watanzania waweze kuona thamani ya pesa zao, shukrani nyingi kwa rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuujenga mradi huu ambao ni wa kielelezo kwa taifa letu,” alifafanua.

About The Author