January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waandishi wa habari wapikwa

Spread the love

UMOJA wa Mataifa (UN) kupitia Taasisi ya Beyond nchini Tanzania umewapika waandishi wa habari kubobea katika masuala ya Mpango wa Maendeleo Endelevu wa 2015 (Sustainable Development). Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Mafunzo hayo yametolewa kwa njia ya warsha iliyoendeshwa na waelekezaji kutoka asasi ya Beyond jijini Dar es Salaam ikilenga kuinua ufahamu wa waandishi wa habari katika kufanikisha malengo mapya yaliyowekwa jijini New York, Marekani pamoja na kumalizika yale Malengo ya Milenia bila ya matokeo ya kuridhisha.

Akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo, Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari Tanzania (SJMC), Dk. Ayub Rioba amesema vyombo vya habari vinahusiana na maendeleo ya sehemu yoyote nchini.

Dk. Rioba amesema ni muhimu serikali ikaweka mkazo kutengeneza mazingira rafiki ya kuwezesha waandishi wa habari kushiriki kutoa elimu kwa umma kuhusu kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu.

“Waandishi wa habari wanaweza kuleta maaendeleo ya jamii, uchumi, na siasa kupitia makala na vipindi vyao, changamoto kubwa ni kupata katiba mzuri itakayolinda uhuru wa wa vyombo vya habari,” amesema Rioba.

error: Content is protected !!