April 8, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bei ya mafuta yashuka duniani

Spread the love

 

BEI ya mafuta duniani imeshuka kwa kasi kubwa kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran, yaliyotangazwa hivi karibuni na kupunguza hofu ya uhaba wa nishati katika soko la kimataifa. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa zinaeleza kuwa mafuta ghafi aina ya Brent yameshuka kwa zaidi ya asilimia 13 hadi 16, na kufikia chini ya dola 100 kwa pipa, kiwango ambacho hakikuonekana katika siku za karibuni tangu kuzuka kwa vita hiyo.

Kabla ya kusitishwa kwa mapigano, bei ya mafuta ilikuwa imepanda hadi zaidi ya dola 110 kwa pipa kutokana na hofu ya kuvurugika kwa usambazaji, hasa baada ya kufungwa kwa njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta ya dunia, maarufu kama Strait of Hormuz.

Makubaliano hayo ya muda ya kusitisha vita kwa takribani wiki mbili yamechangia kurejea kwa matumaini ya utulivu wa usambazaji wa mafuta, huku matarajio yakiwa ni kufunguliwa tena kwa njia hiyo muhimu ya usafirishaji.

Mbali na kushuka kwa bei ya mafuta, masoko ya hisa duniani yameonesha kuimarika, huku wawekezaji wakionyesha matumaini kuwa hali ya uchumi inaweza kuimarika endapo amani itaendelea kudumu.

About The Author

error: Content is protected !!