WAZIRI Mkuu Mwigulu Nchemba ameongoza mazishi ya Marehemu William V. Lukuvi aliyekuwa Mbunge wa Isimani na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).
Mwigulu ambaye alimwakilisha Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amesema hayati William Lukuvi alikuwa ni mshauri kwa wabunge wenzake waliomkuta hivyo ni vyema kumuenzi kwa kuwa watulivu hasa katika kipindi ambacho jimbo linahitaji umakini kumpata mbadala wa Lukuvi ataendelea pale alipoishia.
Aidha amesema serikali inatambua miradi yote inayoendelea katika jimbo la Isimani na kuwahakikishia wananchi kuendeleza ukiwemo mradi mkubwa wa barabara ya Msembe -Iringa ambayo ilikuwa ndio kilio kikubwa cha hayati William Lukuvi.
Mwigulu ameongeza kuwa hayati William Lukuvi alikuwa ni msikivu na mwenye kuwapenda wananchi wake jambo lililomfanya adumu kwa Zaidi ya miaka 30 jimboni kwake jambo limekuwa ni gumu kwa wabunge wengi.
amesema hayati Lukuvi alipenda kujitolea na kusaidia watu wengine na kutamani matokeo mazuri katika kazi zake
Aidha amewataka wananchi kuendelea kuwa na umoja na mshikamano kama alivyoacha hayati Lukuvi ili iwe ni sehemu ya kuendelea kumuenzi.
ZINAZOFANANA
Tume ya Uchunguzi matukio ya Oktoka 29 kufikia kikomo Aprili 3
Polisi wakana maafa mgodi wa Msasa, Geita
Bei ya mafuta yazidi kupaa duniani