March 30, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tume ya Uchunguzi matukio ya Oktoka 29 kufikia kikomo Aprili 3

Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mohamed Othman Chande

Spread the love

 

TUME ya Uchunguzi iliyoundwa kuchunguza matukio ya Oktoba 29 inatarajiwa kufika kikomo ifikapo tarehe 3 Aprili 2026 baada ya kukamilisha kazi ya ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa mbalimbali. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Tume hiyo imefanikiwa kukusanya ushahidi kutoka kwa wadau tofauti, wakiwemo mashuhuda wa matukio hayo, taasisi za umma na binafsi pamoja na nyaraka muhimu zilizosaidia kubaini chanzo, athari na wahusika wa matukio hayo.

Ripoti hiyo inajumuisha mapendekezo kadhaa kwa Serikali, ikiwa ni pamoja na hatua za kisheria dhidi ya wahusika watakaobainika kuhusika na makosa, pamoja na maboresho ya mifumo ili kuzuia matukio kama hayo kujirudia siku zijazo.

Awali, Serikali iliunda tume hiyo kufuatia shinikizo la umma kutaka uchunguzi wa kina juu ya matukio ya Oktoba 29 yaliyosababisha taharuki na maswali mengi kutoka kwa wananchi.

Wananchi wengi sasa wanasubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi huo, wakitarajia haki itatendeka na ukweli kuwekwa wazi.

Tume hiyo inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mohamed Othman Chande na itakuwa na wajumbe wengine 7 ambao ni Profesa Ibrahim Juma, Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Balozi Ombeni Sefue, ambaye ni Mwanadiplomasia na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Mwanadiplomasia na Balozi Radhia Msuya.

Wengine ni Luteni Jenerali Paul Meela ambaye ni Mwanadiplomasia na Balozi mstaafu, Said Mwema (Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Balozi David Kapya, Mwanadiplomasia na Balozi mstaafu na Dk. Stergomena Tax, aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi, na pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

About The Author

error: Content is protected !!