March 13, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama yaamuru Wakazi kumlipa Mil 100 Baba Levo

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemhukumu msanii wa muziki wa rap, Wakazi, kumlipa fidia ya Sh. 100 milioni, mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo na kashfa dhidi yake. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Katika hukumu iliyotolewa tarehe 13 Machi 2026, Mahakama ilibaini kuwa madai yaliyotolewa na mshtakiwa hayakuwa na ukweli na yalikuwa na madhara kwa hadhi na sifa ya mlalamikaji

Kutokana na uamuzi huo, Mahakama imeamuru mshtakiwa kuomba radhi hadharani kupitia vyombo vilevile alivyotumia kusambaza taarifa hizo, kuondoa mara moja taarifa zote za uongo katika tovuti, mitandao ya kijamii, blogu, magazeti na chaneli za YouTube, pamoja na kulipa fidia ya Shilingi milioni 100.

Aidha, Mahakama imetoa amri ya kudumu inayomzuia mshtakiwa kusambaza tena taarifa za uongo au za kashfa dhidi ya mlalamikaji. Pia imeelekeza kuwa kiasi cha fedha kilichoamriwa kulipwa kitatozwa riba ya asilimia saba kwa mwaka kuanzia tarehe ya hukumu hadi malipo yatakapokamilika, huku gharama zote za kesi zikibebwa na mshtakiwa, hivyo kuhitimisha rasmi shauri hilo kwa ushindi wa mlalamikaji.

About The Author

error: Content is protected !!