Katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha mazingira safi na salama kwa wananchi, Meridianbet imetoa msaada wa mapipa ya taka katika maeneo mbalimbali ya mitaa ndani ya wilaya ya Kinondoni. Hatua hii inalenga kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa taka, kupunguza uchafuzi wa mazingira, na kuhamasisha utamaduni wa kuwajibika katika kuhifadhi usafi wa maeneo ya kijamii.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Afisa Mawasiliano wa Meridianbet, Nancy Ingram aliwatambua wafanyakazi wa usafi kama mashujaa wa kimya wanaolinda afya za wananchi kila siku. Alisisitiza kuwa kampuni imeamua kutoa msaada huo kama ishara ya kuthamini mchango wao na kusaidia kuboresha mazingira yao ya kazi, hasa wanapokabiliwa na changamoto za kiafya na kimazingira wanapotekeleza majukumu yao.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Manispaa ya Kinondoni aliipongeza Meridianbet kwa moyo wa ushirikiano na uzalendo. Alieleza kuwa mchango huo ni mfano halisi wa namna sekta binafsi inavyoweza kushirikiana na Serikali katika kuimarisha huduma za jamii na kulinda ustawi wa wafanyakazi wa ngazi ya chini pamoja na wananchi kwa ujumla.
Zoezi hili ni sehemu ya mkakati mpana wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) wa Meridianbet, ambapo kampuni imekuwa ikiwekeza katika miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo elimu, afya, michezo na ustawi wa vijana. Kupitia juhudi hizi, Meridianbet imeendelea kujenga daraja la matumaini kwa jamii na kuonesha dhamira ya dhati ya kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii.
Kwa kuendeleza ushirikiano huu, Meridianbet inadhihirisha kuwa mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na wajibu wa kijamii. Utoaji wa mapipa ya taka katika maeneo ya umma si tu mchango wa kimazingira, bali ni uwekezaji wa moja kwa moja katika afya, hadhi na maendeleo endelevu ya jamii ya Watanzania.
ZINAZOFANANA
Vaso Psycho kuleta mapinduzi mapya ya ushindi kupitia Meridianbet
Kwa taarifa zaidi ingia Meridianbet Sport Portal
Milionea mpya kupatikana kupitia Meridian Jackpot