Tundu Lissu akiwa mahakamani
SHAHIDI wa nane wa Serikali ambaye ni shahidi wa siri aliyepewa utambulisho wa P8 katika kesi Na.19605/2025 inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameeleza Mahakama kuwa yeye alikamatwa Moshi, mkoani Kilimanjaro baada ya kuhamasisha vijana wenzake kufanya uasi dhidi ya serikali. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Kesi hiyo inasikilizwa katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.
Shahidi huyu anadai kuwa tarehe Aprili 2025 akiwa mitaa ya Njoro, Moshi mjini alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa anahamasisha vijana wenzake kufanya uasi dhidi ya serikali.
Shahidi huyu alidai kuwa akiwa kwenye ofisi ya Mpelelezi wa mkoa wa Kilimanjaro RCO ibidi akiri kuwa alikuwa anahamasisha uasi dhidi ya serikali.
Shahidi huyo ameieleza mahakama hiyo kuwa siku hiyo hiyo alipewa dhamana ya kujidhamini mwenyewe
Shahidi huyo aliyejitambulisha mahakamani hapo kuwa ni mfanyabiara wa matunda katika solo la Manyema Mbuyuni eneo Moshi mjini pia aliyeyatambulisha makazi yake kuwa ni Njoro, Moshi mkoani Kilimanjaro.
P8 alidai kuwa anajishuhulisha na siasa ” najishughulisha nayo lakini si kwa undani sana.
Amedai mahakamani hapo kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema.
Anadai kuwa anamfahamu Lissu kama Mwenyekiti wa Chadema ambapo tarehe 4 Aprili 2025 anakumbuka kuwa akiwa katika shughuli zake za kibiashara katika soko la Manyema huku akiwa aliperuzi kwenye mtandao ya kijamii “ndio nilipokutana na tamko la Lissu kwa Sasa ni mshtakiwa kwenye mtandao wa YouTube na Facebook kwa kutumia simu Janka”.
Akitumia simu yake aliona na kusikia kupitia YouTube tamko la Lissu akihamasisha uasi kwamba lazima tufanye uasi dhidi ya serikali.
Kabla ya shahidi huyo wa nane, mapema asubuhi jopo la majaji watatu lilimsikiliza shahidi wa saba wa serikali akitoa ushahidi wake ambaye aliongozwa na Wakili wa serikali Ignas Mwinuka.
Shahidi huyo mwenye umri wa miaka 38 anayejishughulisha na ufundi umeme mkazi wa Matalawe, Songea aliyedai mahakamani hapo kuwa yeye ni mfuasi wa Chadema.
Shahidi huyo amedai mahakamani hapo kuwa anahudhuria sana mikutano na kuchangia Chama hicho.
P2 anadai kuwa tarehe 4 Aprili 2025 akiwa Songea mjini akiwa na shughuli zake akiwa anaperezi kupitia mtandao ya kijamii alimuona Lissu akiwa anahutubia mkutano wa waandishi wa habari
Wakili Ignas: Mtandao gani:
Shahidi P2: YouTube nilikuaa naangalia.
Wakili Ignas: ukabaini nini?
Shahidi P2: Nilikutana na ujumbe wa mwenyekiti wa chama akisema hakutakuwa na uchaguzi, wanaotaka kugombea wasahau mwaka huu. Alisisitiza namna ya kuzuia uchaguzi ni njia ya kuleta mabadiliko na alihamasisha kila mmoja awe jasiri.
Wakili Ignas: ulifanya nini wewe?
Shahidi P2: Nilivyopata ujumbe huo nikapata hamasa na kuanza kuwatafuta viongozi walioko songea ili tujue linatekelezeka vipi hilo.
Wakili Ignas: Kingine kilichoendelea?
Shahidi P2: Nilimtafuta Essau Said Mwenyekiti wa Vijana Songea kwa ufafanuzi zaidi.
“Alinielekeza atafanya mawasiliano na viongozi wengine na ilipofika tarehe 7 Aprili 2025, kwahiyo alituambia tutoe michango ya hiari na mimi nilichangia elfu 10 hiyo michango ya hiari inaitwa Tonetone.
Wakili Ignas: Mwendelezo wa ziara ya mwenyekiti wa Chadema taifa?
Shahidi P2: Niliendelea na shughuli zangu nikawa nasubiri tarehe 10 Aprili 2025 ambayo itakuwa ndio siku ya mkutano na tuliambiwa hivyo sisi.
Shahidi huyo anaeleza kuwa yarehe 9 Aprili alipata taarifa kuwa Lissu alikamatwa na kwa kuwa hakuwa na taarifa za kutoa kesho yake tarehe 10 Aprili alijiandaa kwenda mkutanoni ili kupata ufafanuzi wa nini kimeendelea hadi Mwenyekiti kukamatwa.
P2 anadai kuwa aliona polisi walitanda eneo la mkutano “nikaona nielekee ofisi za chama maana tuliambiwa Makamu Mwenyekiti wa chama atakuwa anazungumza na wanachama pale ofisini.
Wakili Ignas: Makamu Mwenyekiti anaitwa nani?
Shahidi P2: John Heche.
Wakili Ignas: Nini kiliendelea?
Shahidi P2: Tukiwa pale ofisi za chama wakati tunasubiri Heche azungumze wakaja polisi na mimi nilikamatwa katika tukio hilo na kupelekwa kituo cha polisi.
Wakili Ignas: Nini kiliendelea kituoni?
Shahidi P2: Niliwekwa mahabusu na baadae nikahojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo na uchochezi.
Wakili Ignas: Nini kiliendelea?
Shahidi P2: Waliniachia kwa Dhamana na nilitakiwa kuwa naripoti kila jumatatu.
“Tarehe 14 Aprili niliripoti na tare21 Aprili nilipaswa kuripoti tena, ikawa sikukuu nikarudi tarehe 22 Aprili ambapo nilipofika nikapelekwa Central kuchukuliwa maelezo kwa mara ya pili.
Wakili Ignas: Maelezo gani?
Shahidi P2: Akaniambia nieleze mwanzo mwisho hadi nilipokamatwa. Nikamueleza kuwa mimi ni mwana chama na akayachukua hayo maelezo afande Juma Batazary.
Wakili Ignas: Tundu Lissu umemtaja sana unamfahamuje?
Shahidi P2: Nikiwa Songea nimemfahamu Tundu Lissu anafahamika karibu na kila mtu toka akiwa bungeni na alikuwa Makamu Mwenyekiti na baadae akawa Mwenyekiti.
Wakili Ignas: huo uchaguzi ungezuiwaje Kwa mujibu wa Lissu?
Shahidi P2: Sijui ungezuiwaje lakini yeye alisema kwa uasi, mwenyekiti wa vhama alikuwa anakuja Ruvuma na tukajua angekuja kutupatia mbinu hizo maana alisema wanaotaka kwenda nae ataenda nao na mimi nilikuwa kwenye kundi hilo.
Jaji: Shahidi unaongea mfululizo, hatujui unaelekea wapi wala unaongea nini? Sasa Wakili muongozeni shahidi tujue ameanzia wapi na anaelekea wapi?
Wakili Ignas: Ulikuwa unajua uchaguzi utazuiwaje?
Shahidi P2: Nilikuwa sijui.
ZINAZOFANANA
Kesi ya Lissu yaanza kunguruma mahakamani
Lissu alivyombana shahidi wa sita, awasubiri wengine kesho
RITA yatoa mafunzo ya usimamizi wa mirathi, utatuzi wa migogoro kwa Viongozi wa Serikali, wazee wa kimila