February 13, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Lissu avuna kielelezo kingine kutoka serikalini

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

TUNDU Lissu ameendelea kuvuna vielelezo kutoka kwa mashahidi wa Serikali kwenye kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Shahidi huyo wa tano wa jamhuri aliyepewa jina la uficho kwa kuwa ni shahidi wa siri. Utambulisho wake ni ‘P6’. Lissu baada ya kulinganisha maelezo aliyoyatoa polisi na aliyoyatoa mahakamani leo tarehe 13 Februari 2025.

Tayari Lissu anafaida ya vielelezo vitatu alivyovitanguliza mahakamani kutoka alivyovipata kupitia mashahidi wa serikali waliotangulia wakati wakitoa ushahidi wao.

Shauri hilo linalosikilizwa na jopo la majaji watatu wanaongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akishirikiana na wenzake Jaji James Karayemaha, na Jaji Ferdinand Kiwonde.

Lissu alimuuliza shahidi huyo kama maelezo yake yapokelewe kama kielelezo mahakamani hapo alikubali ndio Jaji Ndunguru akiyapa maelezo hayo utambuzi kama kielelezo D4 yaani kielelezo cha nne cha utetezi.

Lissu: Kabla hujaapishwa hapa Mahakamani uliulizwa dini yako ukasema wewe ni Mkristo?

P6: Kweli

Lissu: Waeleze majaji kwenye hayo maelezo yako eneo la dini yako umeweka nini?

P6: Sijaona hapo.

P6: Hapa dini imeandikwa sioni vizuri.

Lissu: Dini imeandikwa muislamu?

P6: Hapa sioni vizuri.

Lissu: Umri wako je?

P6: Miaka 23 imeandikwa hapa.

Lissu: Ulisema shughuli za chama ulizopewa ni kuongoza misafara ya chama ukiwa na bendera na pikipiki?

P6: Ni kweli.

Lissu: Sasa hayo maneno yapo kwenye maelezo yako?

P6: Maelezo yanaonesha nitashiriki kwenye mikutano ni vitu ambavyo sikuviandika.

Lissu: Kwahiyo hayo yameandikwa au hayajaandikwa?

P6: Maelezo yameandikwa kushiriki mikutano.

Lissu: Wewe Chadema wa mapolisi usitupotezee muda, tuambie yapo kama yapo?

P6: Sijui

Lissu: Tarehe 4 Aprili umesema ulikuwa na simu yako infinix smart 8 tuambie kama hayo yapo kwenye maelezo yako?

P6: Sifahamu.

Lissu: Sijakuuliza unayafahamu au huyafahamu, nimekuuliza yapo au hayapo?

P6: Sifahamu.

Lissu: Mheshimiwa Jaji naomba shahidi ajibu maswali yangu.

Jaji: Hebu muulize tena.

Lissu: Hayo maneno ya simu Infinix smart 8 yapo au hayapo?

P6: Sifahamu.

Jaji: Nafikiri lengo lako mshitakiwa ni ku empeach credibility ya shahidi kwahiyo akisema hafahamu wakati kielelezo kipo na sisi Mahakama tutakipitia. Basi acha aendelee kusema hafahamu.

About The Author

error: Content is protected !!