Mwenyekiti ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman
MAHAKAMA Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2025 katika majimbo 17 ya Unguja lililofunguliwa na wagombea wa majimbo hayo kupitia Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 13 Februari 2026, na Jaji Salma Ali Hassan ambaye amesema kuwa shauri hilo limekosa miguu ya kisheria kwa sababu viapo vilivyoendana na maombi yao havikuandaliwa na wakili mwenye leseni ya kulisha viapo.
Aidha uamuzi huo unatokana na pingamizi liliwasilishwa mahakamani hapo na mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Baada ya uamuzi huo Mwanasheria Mkuu wa ACT, Omar Said Shaaban, amesema wanafungua maombi upya ikiashiria msimamo wao kwamba mapambano yanaendelea.
ZINAZOFANANA
Lissu avuna kielelezo kingine kutoka serikalini
Kesi ya Lissu yaanza kunguruma
Mahakama: Kumnyima chakula Lissu ni kukiuka haki za binadamu