Tundu Lissu akiwa mahakamani
MAHAKAMA Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imeamuru kufanyiwa marekebisho kwa kizimba kinachotakiwa kutumiwa na shahidi wa siri ili aweze kuonekana na majaji wakati wa utoaji ushahidi. Anaripoti Fedrick Gama, Dar es Salaam … (endelea),
Maelekezo hayo yametolewa leo 11 Februari 2026, wakati wa usikilizwaji wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, anayeshtakiwa kwa kosa la uhaini.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mwenendo wa usikilizwaji wa kesi unakwenda kwa uwazi kwa upande wa jopo la majaji, huku utaratibu wa kumlinda shahidi ukiendelea kuzingatiwa kwa mujibu wa taratibu za mahakama. Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea katika mahakama hiyo.
Tayari upande wa serikali umeshawasilisha mashahidi watatu, akiwemo George Bagyemu, Naibu Mkuu wa upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (D-ZCO), John Kaaya, Mpelelezi kwenye doria ya mtandaoni, na Samweli Kaaya mtaalamu wa uchunguzi wa picha.
Shauri hilo lilioanza tarehe 10 Aprili 2025, kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kama mahakama ya kabidhi (committal Court), na baadaye shauri hilo kuhamia mahakama kuu tangu Julai mwaka jana.
Lissu ana siku 309 gerezani katika Gereza Kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam ambapo yeye mwenyewe amelalamikia kudorora kwa mwenendo shauri hilo kutokana na kuchelewa kwa shauri hilo.
Lissu ameongeza. “Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokiukwa. Justice delayed is justice denied”.
Lissu ameongeza “Katiba yetu inaelekeza Mahakama ziendeshe mashauri kwa namna ambayo haitachelewesha Haki. Ibara ya 147 ya Katiba inasema”
Lissi amenukuu kifungu cha 5 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinasema mashauri yanaendeshwe kwa haraka.
Lissu ametaja kuwa changamoto za kudorora kwa mwenendo wa shauri dhidi yake unatokana na kuendeshwa kwa mtindo wa vikao “Tatizo lipo kwenye utaratibu wa session ndio tatizo na hilo ni tatizo la wanaoamua kesi iendeshe kwa njia ya session”
Mwanasiasa huyo ameisomea mahakama hiyo kilichoandikwa kwenye ripoti ya haki jinai ya 2-23 ukurasa wa 17 na 18 kuhusu vikao vya mahakama kuu (High Court Session) tume inasema uendeshaji wa mashauri kwa njia ya vikao huchelewesha mashauri hayo. “Kati ya mashauri 2000 ni mashauri 700 tu ndio yalisikilizwa pekee kwa mtindo wa session.”
“Hivyo basi uendeshaji wa kesi kwa kutumia session unaamuriwa na Jaji Mkuu zikiisha siku tunasubiri aseme tena ndo maana zimepita siku 88 bila kesi hii kuendelea hadi atakapopanga tena huyo Jaji Mkuu”.
Ameeleza kuwa ucheleweshaji huu sio kosa la majaji wala mawakili wa Serikali ni kosa la utaratibu uliowekwa uliwekwa .
“Leo hapa High Court Dar es salaam kuna majaji wakutosha lakini ili kesi yangu isikilizwe lazima Jaji atoke Songea, mwingine Mtwara sijui na lazima walipwe, Usafiri, Chakula na kila kitu”
“Usipowalipa kesi haiendelei na mimi mtuhumiwa nateseka huko jela. Walishindwa nini kuwapangia majaji wa hapa ili kesi isikilizwe kila siku.”
Lissu ameongoza “Zamani majaji walikuwa wachache sana lakini siku hizi kila mkoa kuna majaji. Nashangaaa mambo haya kwa utaratibu huu sasa”
Lissu amedai kuwa shtaka la uhaini ndio kosa kubwa zaidi nchini. “Hili ni kosa la kipekeee, angalieni ibara ya 28(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndo kosa pekee la jinai lililotajwa kwenye katiba kwasababu sio kosa la kawaida,”.
“Kama hiyo ndio hoja kosa hili pia la Uhaini linapaswa kuwa na kipaumbele maana ni tofauti na makosa mengine yote,” alidai Lissu.
Amezitaja kesi mbili za uhaini zilizowahi kutokea nchini “kwenye kuthibitisha hilo hii sio kesi ya kwanza ni kesi ya tatu toka tumepata uhuru. Kesi ya Grey Likungu miaka 56 iliyopita ilikuwa na washitakiwa 9 lakini ilichukua miezi 6 tu hadi kufika Mahakama ya rufani.”
“Kesi nyingine ni kesi ya Khatib Gandi na wenzake 18 kutoka Mahakama Kuu hadi Court of Appeal kuanzia ilipoanzia hadi ilipoishia ilichukua miezi 14 na mashahidi 140. Sisi tuna miezi 10 tumemaliza mashahidi watatu tu”
“Vyovyote itakavyokuwa kesi hii inachukuliwa kama kesi ya kawaida ya jinai. Haiwezi chukuliwa poa hata kidogo lazima hili lieleweke vizuri.
“Kwa utaratibu huu tutafika mwaka 2030 kama mtakuwa hamjastaafu bado kwa spidi hii ya miezi 10 mashahidi watatu”
“Sasa kesi ya Grey Likungu Mataka ilisikilizwa na Jaji mmoja na kesi ya Khatib Gandi Ilisikilizwa na Jaji mmoja pia.
Kesi ya tatu Jaji Mkuu anasema mmoja hawezi ndio maana anawateua muwe watatu kusikiliza kesi hii.”
“Kwenye kesi hii Jaji mkuu asipowatumieni hela hamji. Kesi hii ina ugumu gani hadi muwe watatu?” alihoji”.
ZINAZOFANANA
Dk. Homera azitaka bodi za Udhamini kujiepusha na ubadhirifu wa mali za umma
DED Yegella: Fedha za ndani kunufaisha kata zote Mbeya DC
Mtihani mpya wagubika kesi za uwakilishi