NDEGE moja ya kiraia iliyokuwa na watu 55 imetua baharini karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde mjini Mogadishu, baada ya rubani kufanya uamuzi wa kutua karibu na ufuo kufuatia hitilafu ya kiufundi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taatifa zinasema, abiria na wafanyakazi wote wameokolewa salama.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia imesema ndege hiyo ilipaa kutoka Mogadishu kuelekea Galkayo, mji mkuu wa mkoa wa Mudug, wakati hitilafu iliporipotiwa muda mfupi baada ya kupaa na marubani waliomba kurejea.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Ahmed Macalin Hassan, ndege hiyo ilitua lakini haikuweza kusimama kwenye barabara yake, na kuelekezwa hadi eneo la baharini karibu na uwanja wa ndege.
Abiria wapatao 50 na wafanyakazi watano walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Vikundi vya kutoa msaada vilitumwa mara moja, na watu wote 55 walihamishwa hadi eneo salama. Hakuna vifo au majeraha makubwa yaliyoripotiwa.
Shirika la ndege, Starsky, lilisema limeanzisha uchunguzi kuhusu tatizo la kiufundi na kupongeza uamuzi wa kijasiri wa rubani kutua karibu na bahari, ikibaini kuwa hatua hiyo ilikuwa muhimu katika kuokoa maisha ya watu wote ndani ya ndege hiyo.
Maafisa wa usafiri wa anga wanasema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini sababu hasa na kutathmini athari zozote kwa usalama wa ndege.
ZINAZOFANANA
Tanzania kujisogeza Ulaya, Zungu apiga hodi Serbia
Rais Museven kuwasili Tanzania kesho kwa ziara ya kikazi
Rais Kiir ateuwa aliyekufa miaka 5 iliyopita kusimamia uchaguzi