February 10, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Serikali kujibu hoja za Lissu, kumpinga shahidi wa siri kesho

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

NI siku 88 tangu kuahirishwa kwa shauri la uhaini Na. 19605/2025 linalomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho tarehe 9 Februari shauri hilo linaendelea kusikilizwa mfululizo mpaka tarehe 6 Machi 2026. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu aliibua pingamizi la uhalali wa kutumika kwa sheria ya kulinda mashahidi akidai kuwa sheria hiyo haijachapishwa kwenye gazeti la Serikali na kwamba sheria yoyote ambayo haijachapishwa kwenye gazeti hilo haiwezi kutumika.

Lissu ameibua pingamizi hilo tarehe 12 Novemba mwaka jana ambapo shahidi wa nne wa serikali ambaye ni wa siri aliyepewa jina la ‘p1’ alipotaka kuanza kutoa ushahidi wake.

Lissu alidai mahakamani hapo kuwa hata kama sheria ya ulinzi wa mashahidi ingekuwa halali kutumika basi shahidi huyo alitakiwa kuonwa na majaji lakini hata majaji wanaendesha shauri bila kumuona shahidi jambo ambalo Lissu amedai halikubaliki kisheria.

About The Author

error: Content is protected !!