Wanafunzi wa darasa la saba wakifanya mtihani
BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika kuanzia 17 Novemba 2025,Matokeo hayo yametangazwa leo Jumamosi 31 Januari 2026 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Profesa Said Mohammed. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa matokeo hayo, jumla ya watahiniwa 526,620 kati ya 595,810 waliopata matokeo wamefaulu mtihani huo, hatua inayodhihirisha ongezeko la ufaulu kwa mwaka huu.
Takwimu zinaonesha kuwa ufaulu umepanda kwa asilimia 2.61 na kufikia asilimia 94.98 ambapo watahiniwa 526, 620 wamefaulu kwa kupata daraja I,II, III na IV.
Kati ya watahiniwa wa shule 569,914 waliosajiliwa mwaka 2025, wavulana ni 266,024 sawa na asilimia 47 na wasichana ni 303,859 sawa na asilimia 53.
Aidha Said Mohammed amesema wanafunzi 77 wamefutiwa matokeo ya kidato cha 4 kwa sababu za kuandika lugha chafu na wengine kwa udanganyifu katika mtihani kati ya hao 47 kutoka kwenye vituo vya mtihani na 30 kutoka shule huku mahudhurio katika mtihani huo yalikuwa asilimia 97.5 sawa na wanafunzi 555,606.
ZINAZOFANANA
Uwekezaji wa Samia, wanafunzi 16 wasomea Data Science na AI Afrika Kusini
Meridianbet yawakumbuka wanaopitia maisha magumu Kinondoni
Wizi wa michango ya Lissu: Chadema hakihusiki – Familia