Jaji Julius Mallaba
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kwa familia, ndugu na jamaa wa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Julius Mallaba, aliyefariki dunia Ijumaa ya tarehe 19 Desemba 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Jaji Mallaba amekutwa na mauti wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Alikuwa akisumbuliwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu.
Jaji Julius Benedicto Mallaba, alizaliwa tarehe 12 Machi 1960. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, tarehe 25 Julai 2015.
Alistaafu rasmi tarehe 12 Machi 2020 baada ya kufikisha umri wa ukomo wa utumishi wake serikalini.
Wakati wa uhai wake, Jaji Mallaba, aliwahi kuwa mwanasheria katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
ZINAZOFANANA
Serikali iko tayari kusikiliza, ili kulinda umoja – Simbachawene
Chadema: Tutaishitaki Magereza kuminya Lissu haki zake
Mihemko ya madereva chanzo za ajali za mwisho wa mwaka