Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema, Serikali itaendelea kuthamini na kushirikiana na viongozi wa kiroho na kidini katika kujenga taifa linaloheshimi haki, amani, usalama na mshikamano wa kitaifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza jana Jumapili, wilayani Karagwe mkoani Kagera, mkoani Kagera, Simbachawene alisema, madhehebu ya kidini, ni wadau muhimu wa ujenzi wa taifa linalozingatia haki.
Alikuwa akihutubia kwenye ibada ya Ubarikio wa Uchungaji wa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe.
Katika ibada hiyo, mashemasi watano walibarikiwa na kuingia rasmi katika huduma ya kichungaji.
Alisema, “Serikali iko tayari kusikiliza maoni, kujifunza na kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa dini. Ninawaomba Watanzania kuwa wavumilivu, ili kulinda na kuendeleza amani, umoja na mshikamano wa taifa.”

Waziri huyo wa mambo ya ndani ametoa kauli hiyo, wiki moja baada ya kulitaka jeshi la polisi, kufuata taratibu wakati wa kukamata watuhumiwa. Amekuwa akikemea vitendo vya utekaji na utesaji, vilivyoshamiri kwa kasi nchini.
Naye Askofu wa Dayosisi hiyo ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia misingi mitano ya maridhiano, kufuatia matukio yaliyotokea 29 Oktoba 2025.
Akamiza jamii kuendeleza mazungumzo, msamaha na mshikamano, ili kuwapo amani ya kudumu.
Kwa mujibu wa Askofu Bagonza, taifa limegawanyika kufuatia matukio ya kabla na baada ya uchaguzi wa 29 Oktoba na kuongeza kuwa “njia pekee ya kuliponya taifa, ni kuwapo mazungumzo yenye dhamira ya kulirejesha taifa lilipokuwa.”
ZINAZOFANANA
Samia atuma salamu za pole kwa Jaji Mallaba
SADC watua nchini kushughulikia mgogoro wa kisiasa
Chadema: Tutaishitaki Magereza kuminya Lissu haki zake