March 13, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dawasa yawapa matumaini wakazi wa Dar suala la maji

Mhandisi Mkama Bwire

 

WAKATI wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakilalamika shida ya maji, afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire, amesema kuwa changamoto hiyo inatokana na hali miinuko inayosababisha maji kushindwa kufika maeneo hayo. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema hayo leo tarehe 12 Desemba 2025 alipokuwa akijibu swali lilihoji juu ya changamoto ya maji maeneo mengi jijini hasa Kimara .

“Utofauti uliopo kati ya maeneo yaliyo inuka na yaliyo chini na ukizingatia idadi ya watu waliovuta maji katikati inapelekea changamoto katika upatikanaji wa maji meneo la kimara,” amesema Mhandisi Bwire.

Amesisistiza kuwa wakati huu wameboresha eneo la huduma kwa wateja ili kuwepo na urahisi wa kupokea malalamiko na kwa haraka kwakuwa wakati mwingine mtu hapati maji akihisi yamekatika kumbe ni mita ndio inatatizo.

Hata hivyo Mwandishi wa habari hizi amezungumza na baadhi ya wakazi wa Kinondoni, ambao wamesema kuwa mitaa hiyo haina maji.

“Kusema kweli watu wenye visima ndio wanaotusaidia hakuna maji tukiuliza tunaambiwa jua kali ndio linalosababisha hali hii” alisema mmoja wa wakazi wa Kinondoni.

About The Author

error: Content is protected !!