Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba
TANGU Desemba 9, 1961 Tanganyika ilipopata uhuru wake, siku hiyo imekuwa ni ya kipekee kwa wananchi ambapo hukumbuka uhuru wa taifa lao. Anaripoto Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Kumbukumbu hiyo huendana na sherehe za kitaifa zinazofanyika katika uwanja uliochaguliwa na serikali. Hapo wananchi hupata kuona vikosi vya ulinzi na usalama wa raia na mali zao vikifanya gwaride kwa namna ya kipekee.
Ni miaka 64 sherehe hizo zimekuwa za mvuto wa iana yake ingawa mara chache serikali ilitangaza kufutwa ka sherehe hizo na kuelekeza fedha zilizotengwa kwa ajili hiyo kutumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi fulani wenye tija kubwa kwa wananchi.
Ni siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sana sit u na wananchi bali hata askari wanaoshiriki gwaride kwa kuwa wanataka kuonyesha ukakamavu wao na mbwembwe kwa wananchi wanaogharimia uwepo wao.
Mwaka huu, mambo ni tofauti kabisa, hakuna mwenye kutamani siku hiyo ifike. Si kwa askari, raia wala viongozi. Badala ya furaha iliyozoeleka sasa imekuwa hofu. Serikali inawashauri watu wapumzike majumbani mwao.
Siku ambayo ilikuwa ikitumiwa na baadhi ya watu kwenye kwenye fukwe, nyumba za starehe na matembezi mafupi sasa imekuwa ‘baki nyumbani’ kwa usalama wako.
Mitaani wanajeshi na askari wamejaa wakirandaranda kujiweka tayari kukabiliana na maandamano yaliyotangazwa kufanyika kesho bila kibali cha jeshi la Polisi.

Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba ametoa tahadhari kuwa kesho watu watulie majumbani mwao isipokuwa kwa wale ambao watalazimika kutoka kutokana na majukumj yao ya kikazi.
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene ,ametoa onyo kali kwa wananchi kutoshiriki maandamano na kudai kuwa “mtu anayeshabikia maandamano hayo hana uzalendo kwa nchi yake wala haipendi Tanzania”
Hii Tanzania inayozungumzwa hivi sasa ni matokeo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika tarehe 26 Aprili, 1963.
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, leo tarehe 8 Desemba, 2025 akiwa jijini Dar es Salaam, amewaeleza wandishi wa habari maandamano yaliyoitishwa si halali kwa kuwa hayana kibali, hawafahamiki waandaaji wake, hayafuati utaratibu, na hayana mwisho.

Kwa maelezo yake si halali na yanaonyesha dalili za uvunjifu wa amani na hata viashiria vya mapinduzi.
Kutokana na matamko mbalimbali yanayotolewa na mamlaka kuhusiana na maandamano ya tarehe 9 Desemba, Mwanahalisi tv imeingia barabarani kuangalia hali hali ya usalama ilivyo katika jiji la Dar es Salaam. Mambo ni tofauti na siku nyingine na hakuna foleni.
Hali ni shwari na ulinzi ukiwa umeimarishwa si kwa kutegemea askari polisi na wale wa usalama barabarani (trafiki) bali sasa wameongezeka na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Katika mazingira haya, Desemba 9 ni furaha au hofu? Ni huzuni au tabasamu. Nini kifanyike kuirejesha Tanzania tuitakayo?
ZINAZOFANANA
Hakuna tishio la kuzima mtandao nchini – Simbachawene
Jaribio la Mapinduzi Benin lazimwa
Serikali ya Benin imepinduliwa